Kampuni za Uhasibu Zilizosajiliwa

Kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 8 (2) cha sheria ya Uhasibu na Wakaguzi (usajili) [ Sura ya 286 R.E 2002], Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA anatakiwa kuchapisha orodha ya makampuni ua Uhasibu yaliyosajiliwa; Uchapishaji utakaofanywa chini ya sharti hili ni uthibitisho kuwa mtu au kampuni waliotajwa humo wamesajiliwa chini ya sheria hii.

Kwa hiyo ni kosa chini ya kifungu cha 29 kuajiri mtu yeyote au kampuni ambayo haijasajiliwa na Bodi.

Umma pamoja na kampuni zinatakiwa kuthibitisha kuwa wahasibu wamesajiliwa NBAA kabla ya kuwaajiri ili wasikiuke masharti ya sheria.

Bofya HAPA kupata orodha ya kampuni za uhasibu zilizosajiliwa na NBAA kama ilivyokuwa 1 Mei, 2019