Taarifa kwa Umma: Tanzia

Imewekwa: Nov 10, 2024


Tunasikitika kutangaza kifo cha CPA Method Kashonda aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa zamani na mwana Taaluma nguli wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) aliyefariki tarehe 9/11/2024 wakati akishiriki matembezi ya hisani kuchangia vitabu vya kufundishia masomo ya biashara na hesabu kwa shule za sekondari nchini.

Matembezi hayo yameandaliwa na Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) na NBAA ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Uhasibu duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 10 Novemba duniani kote.

Mzee Method Kashonda alianguka ghafla dakika chache baada ya kuanza matembezi. Alikimbizwa hospitali ya Muhimbili kwa bahati mbaya umauti ukamkuta.

Tunatoa pole kwa familia ya CPA Method Kashonda, wana taaluma wote wa Uhasibu na Taifa kwa ujumla kwa kuondokewa na mtu shupavu na mahiri aliyepambana kwa bidii kuiendeleza na kuipeleka mbele taaluma ya Uhasibu kitaifa na kimataifa.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Imetolewa na:

CPA PIUS MANENO

MKURUGENZI MTENDAJI NBAA

9/11/2024