Historia

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ni Taasisi inayosajili na kusimamia Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu na kudhibiti taaluma ya Uhasibu nchini. NBAA Ilianzishwa kwa sheria ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu sura ya 286 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002. Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu ipo chini ya Wizara yenye dhamana ya fedha. Bodi ilianzishwa mwaka 1972 na kuanza kufanya kazi zake rasmi kuanzia tarehe 15 Januari 1973.

Tangu kuanzishwa kwake, NBAA imetoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taaluma ya uhasibu nchini Tanzania hasusani katika kuhamasisha, kusajili, kuwekaji viwango na usimamizi wa mitihani. NBAA inajitahidi kutoa mchango mkubwa katika kuhamasisha utawala bora kupitia uendelezaji wa taaluma ya uhasibu nchini Tanzania.

Taaluma ya uhasibu ina mchango muhimu katika kuchochea kujiamini kibiashara na kusaidia ukuaji wa kiuchumi. Wanachama wa NBAA wanatoa mchango mkubwa wa kushawishi sekta ya umma na binafsi kama chombo cha kitaalamu. NBAA pia inasaidia wanachama na wadau kwa njia ya huduma mbalimbali na kutoa sauti ya pamoja kwa taaluma.