Accounting Technician (AT)
Ili kukamilisha usajili, kwenye kundi hili, mtu anatakiwa kujaza fomu ya maombi iliyopo kwenye tovuti na ambatisha yafuatayo:
Nakala ya cheti cha Bodi cha Accounting Technician (ATEC) au kinachofanana na hicho.
Uthibitisho wa kupata uzoefu kwa vitendo unaotakiwa katika uhasibu (maelezo ya mwajiri).
Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi isiyorudishwa na
Mdhamini mmoja Mhasibu.
Mwombaji akifanikiwa kujaza fomu atataarifiwa baada ya idhini ya Bodi na kupewa cheti cha uanachama.
Tafadhali embelea mfumo wa usajili wa mwanachama na wanafunzi (MEMS) kwa maelezo zaidi.