Temporary Associate Certified Public Accountant ( TACPA )
“Mwanachama wa muda” maana yake ni mtu ambaye si raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na mwenye sifa ya kusajiliwa na Bodi na ambaye ametimiza masharti kama yanavyoelezwa kwa ajili ya usajili huo.
Mgeni ambaye si raia ni lazima ajaze fomu ya maombi ya usajili wa Mhasibu;CPA/ACPA-PP fomu iliyopo kwenye tovuti na aambatishe vifuatavyo: -
Nakala zilizothibitishwa za vyeti husika vliivyotolewa na taasisi/Bodi ya Uhasibu chenye hadhi sawa kilichopo nje ya Tanzania;
Jina na anwani vya mwajiri kuwa kama mdhamini;
Wadhamini wawili Wahasibu waliosajiliwa na Bodi (ACPA au FCPA);
Uthibitisho wa ajira na mwajiri nchini,
Picha mbili za pasipoti za mwombaji zilizopigwa hivi karibuni
Uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi iliyoelezwa na isiyorudishwa.
Kusaini ahadi kuwa baada ya usajili, mtu huyo atatimiza masharti ya Sheria, Sheria ndogo, kanuni na maelezo mengine yanayotumika, na kutotumia cheo au barua ya utambulisho kabla ya kusajiliwa au baada ya kukoma kuwa mwanachama aliyesajiliwa, na kuahidi kufuata kwa ukamilifu kanuni za maadili ya kazi zilizotolewa na Bodi.
Bodi, baada ya kupitia na kuzingatia maombi, kwa mujibu wa kanuni hii, itampa mwombaji aliyefanikiwa cheti cha usajili wa muda kuwa Certified Public Accountant au inawezaa kuwa certified public accountant in public practice.
Baada ya kufanikiwa kusajiliwa na Bodi, mwanachama aliyesajiliwa kwa muda nje ya Afrika Mashariki ni lazima afanye mitihani na kufaulu mitihani miwili ya utozaji kodi nchini na sheria ya kampuni katika kipindi cha miaka miwili baada ya kusajiliwa, na katika masharti mengine kadri Bodi itakavyoamua kila baada ya muda.
ZINGATIA: kwasasa, taarifa zote kuhusu usajili na kupanda daraja, zinapatikana kupitia mfumo wa usajili wa wanachama na wanafunzi (MEMS).