Taratibu za usajili
Usajili wa Watahiniwa
Watahiniwa wanaotarajia kujisajili kwa ajili ya mitihani ya Bodi wanatakiwa kujaza Candidacy Registration Form. Form hii ni lazima ijazwe kwa ukamilifu na kuwasilishwa Bodi pamoja na vyeti vinavyohusika. Vyeti vya masomo na vyeti vya kitaaluma, vikiambatanishwa na matokeo ya mitihani pamoja na picha tatu za pasipoti za rangi. [Kwa sasa utaratibu huu hufanywa kwenye mfumo wa usajili wa wanachama na wanafunzi, (MEMS) unaopatikana katika tovuti hii.]
Bodi imeweka masharti ya chini kabisa ya kujiunga yatakayo mwelekeza mtahiniwa kutambua alama zake za kujiunga na mitihani kutegemea sifa za awali zilizopatikana mwanzo.
Maombi ya msamaha
Bodi hutoa msamaha kwa sehemu za mitihani yake. Msamaha huu unasimamiwa na Sera ya msamaha ya NBAA kuwa na sifa za kusamehewa, mtahiniwa ni lazima ajaze sehemu ya msamaha kwenye fomu ya usajili wa utahiniwa.
Maombi ya msamaha ni lazima yakamilishwe kabla ya kuanza kiwango ambacho msamaha unaombwa. Hata hivyo, mtahiniwa atafikiriwa upya kwa msamaha iwapo atawasilisha sifa ya ngazi ya juu, kwa sifa zilizopatikana nchi za nje ya Tanzania waombaji wanatakiwa kuwasilisha maelezo ya muhtasari wa masomo na matokeo kwa ajili ya mtihani anaotaka kufanya. Mtahiniwa hana budi kuwasilisha maombi ya msamaha angalau miezi miwili kabla ya tarehe ya mwisho ya maombi ya mtihani anaokusudia kufanya.
Pia ni muhimu kuonesha uthibitisho kuwa Chuo Kikuu au Taasisi iliyotoa sifa hizo ni taasisi iliyotambuliwa rasmi. Uthibitisho huu ni lazima upatikane kutoka Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) au Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE) au taasisi nyingine muhimu za kitaaluma.
Tarehe ya mwisho kwa usajili wa mtahiniwa
Mtahiniwa mtarajiwa anaweza kusajiliwa wakati wowote wa mwaka, hata hivyo, kuna haja ya kuzingatia tarehe mtahiniwa anayotaka kufanya mtihani ili aweze kutumia maombi ndani ya tarehe zilizotajwa.
Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha fomu ya usajili wa mtahiniwa ni 15 Februari kwa mitihani ya Mei na tarehe 15 Agosti kwa mitihani ya Novemba hii ni bila faini
Usajili wa kuchelewa
Maombi yaliyopokewa baada ya tarehe za kufungwa kwa maombi yanastahili ada ya kuchelewa.
Kuondoa usajili
Mtahiniwa anaweza kuondoa usajili kwa ridhaa yake au kama alivyoelezwa kwenye sheria ndogo za mafunzo na mtihani.