Masuala yaliyo wazi kutolewa Maoni
Ili kuhakikisha ushirikishaji wa wadau mbalimbali katika mchakato wa kuweka viwango, pamoja na masuala mengine yanayojitokeza siku hizi, Bodi, inaomba maoni ya wadau kwa lengo la kukusanya, kuchanganua na kuwatambulisha bodi zinazoweka viwango na mamlaka husika. Masuala ya taaluma ya uhasibu yanayojitokeza yanaweza kujumuisha Rasimu za kujiweka wazi, makala ya Ushauri na mengineyo yanayohusu maeneo kama vile:-
1.Viwango vya Utoaji, Taarifa za fedha vya Tanzania (TFRS)
2.Viwango vya Utoaji, Taarifa za fedha vya Kimataifa (IFRS)
3.Viwango vya utunzaji, hesabu za sekta ya Umma vya Kimataifa (IPSAS)
4.Viwango vya Kimataifa kuhusu Ukaguzi wa Hesabu (ISAs)
5.Utoaji wa Taarifa Jumuishi wa Kimataifa (IIR)
6.Shirika la Kimataifa la Taasisi za ukaguzi wa Hesabu zenye Mamlaka ya juu (INTOSAI) na maeneo mengine yanayohusiana na taluma ya uhasibu