Ada ya mchango wa mwaka

Kwa mujibu wa Sheria ndogo za NBAA, kila mwanachama atalipa ada ya mchango wa mwaka kuanzia tarehe 1 Julai ya kila mwaka mpaka tarehe 30 Septemba bila faini. Baada ya hapo faini hutozwa kwa atakaechelewa kulipa kwa viwango tofauti vya faini kwa utaratibu ufuatao:-

1.Baada ya miezi mitatu tangu tarehe ya kutakiwa kulipa ipite; adhabu ya faini ya asilimia 25 ya ada iliyotakiwa;

2.Baada ya miezi sita, tangu tarehe ya kutakiwa kulipa, ipite adhabu ya faini ya asilimia 50 ya ada iliyotakiwa

3.Baada ya miezi tisa tangu tarehe ya kutakiwa kulipa, ipite adhabu ya faini ya asilimia 75 ya ada iliyotakiwa; au

4.Baada ya miezi kumi na mbili tangu tarehe ya kutakuwa kulipa, ipite adhabu ya asilimia 100 ya ada iliyotakiwa.

Mtu anayeshindwa kulipa ada ya mchango wa mwaka iliyoelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo atafutiwa uanachama na Bodi.

JEDWALI LA VIWANGO VYA ADA YA MCHANGO WA MWAKA KWA MTU BINAFSI

AT

TZS 40,000

GA

TZS 120,000

ACPA & FCPA

TZS 180,000

ACPA-PP & FCPA-PP

TZS 180,000

AP

TZS 50,000

TACPA

SAWA NA USD 800

TACPA-PP

SAWA NA USD 900

VIWANGO VYA ADA YA MCHANGO WA MWAKA KWA KAMPUNI

KAMPUNI NDOGO

TZS 600,000

KAMPUNI ZA KATI

TZS 1,500,000

KAMPUNI KUBWA

TZS 4,000,000

Taarifa za mwanachama zinapatikana kupitia mfumo wa usajili wa wanachama na wanafunzi (MEMS) unaopatikana kupitia tovuti hii.