Cheti cha IPSAS

Kozi ya Cheti cha IPSAS inawakilisha usimamizi wa fedha za umma hapo baadaye ikisaidia Serikali na raia kupata taarifa muhimu na za wazi kuhusu madhara ya kifedha ya uamuzi wa kulazimisha. Cheti cha IPSAS kitasaidia kuelewa hali ya kifedha ya Serikali na kuwezesha mashirika ya Sekta ya umma: -

Kuwasilisha mtazamo wa kuridhisha wa utendajikazi wa kifedha wa Serikali.

Kuboresha utoaji wa taarifa za fedha za maongezeko kwa Serikali na mashirika ya umma.

Kupata viwango linganishi kwenye huduma kupitia mfumo wa utoaji wa taarifa za fedha za maongezeko kihasibu.

Malengo ya Kozi

Lengo la cheti cha IPSAS ni kuwapa wanafunzi maarifa ya msingi ya baadhi ya viwango vilivyopitishwa, maelekezo ya kiufundi kwa muhtasari na nyaraka muhimu zinazohusiana. Pia kutoa msingi madhubuti wa kuelekea kwenye Diploma ya IPSAS.

Walengwa

Cheti cha IPSAS kitawafaa:

Wale wenye maarifa ya utunzaji vitabu vya fedha kwa maingizo mawili au maarifa ya msingi ya uhasibu.

Sifa za kujiunga

Wenye ATEC II, Diploma ya uhasibu, Shahada ya kwanza katika – Uhasibu, fedha au masomo yoyote ya biashara yanayohusiana.

Muda wa kozi

Muda wa kozi ni miezi Sita. Mitihani itafanywa mara mbili kwa mwaka yaani Februari na Agosti. Mtahiniwa atatakiwa amalize kozi yake ndani ya miezi hiyo sita.

Saa za mawasiliano

Mara mbili kwa wiki Jumanne na Alhamisi kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 1:00 usiku

Ada

Ada ya maombi 20,000/=

Ada ya mafunzo 700,000/=

Ada ya mtihani 300,000/=

Jumla 1,020,000/=

Mahali

Dodoma

Dar es Salaam

Tunzo za NBAA

Mtahiniwa ambaye atafanikiwa kumaliza kozi na mitihani, atapewa cheti cha IPSAS.