Maktaba
Katika kutekeleza moja ya majukumu yake ya kuhamasisha na kutoa nafasi na mazingira bora ya kujisomea kwa masomo ya uhasibu, ukaguzi na masomo yanayoendana na hayo, Bodi ilianzisha Maktaba yake mwaka 1975 kwa lengo la kutoa nyenzo za kujifunzia kwa watahiniwa wanaojiandaa kufanya mitihani yake, wakufunzi, watafiti na wadau wengine.
Dira na Dhamira ya Maktaba
Dira ya mkataba ni kuwa mtoa huduma za taarifa za uhasibu na ukaguzi inayoongoza nchini.
Dhamira ya maktaba ni kutoa huduma bora zinazotosheleza mahitaji ya taarifa kwa ajili ya kujifunza, kufundisha, utafiti, mafunzo na kazi za uhasibu, ukaguzi na masomo yanayoendana na hayo nchini Tanzania.
Malengo ya Maktaba
Malengo ya maktaba ni:-
1. Kujenga mkusanyiko mahususi kutimiza mahitaji ya taarifa ya wanafunzi, walimu na watafiti na kutoa taarifa za hivi karibuni na huduma ya haraka kwa watumiaji.
2. Kutoa huduma na utaalamu uliokusudiwa hasa kuhimiza matumizi yenye ufanisi wa rasilimali za maktaba na taarifa zikiwemo ufundishaji wa stadi za ushughulikaji wa taarifa zinazohamishika.
3. Kuwa mstari wa mbele katika teknolojia za habari za kisasa na kupitia teknolojia hiyo kutoa taarifa za hivi karibuni kwa kushirikiana na kuhusiana na kanzidata za Maktaba nyingine za nje kuhusu uhasibu, ukaguzi na masomo shirikishi ili kuboresha huduma zake.
Machapisho ya Maktaba
Maktaba ina takribani machapisho 10,000 hasa ya vitabu, majarida machapisho ya Serikali, makala za warsha, semina na machapisho mbalimbali za NBAA.
Huduma za maktaba
Kwasasa Maktaba inatoa huduma zifuatazo:-
Huduma ya mrejeo kwa watumiaji wa maktaba- Hii husaidia watumiaji kupata nyenzo za uhasibu, ukaguzi na masomo yanayoendana na hayo
Huduma ya utambuzi- Maktaba huwajulisha mara kwa mara watumiaji wake juu ya machapisho ya sasa yaliyotoka. Machapisho hayo hupatikana kwa kununua, zawadi ama kubadilishana.
Uanachama
Wanachama wa Maktaba ni:-
- Wanafunzi waliosajiliwa kwa mitihani ya Bodi
- Wanachama wenye CPA
- Wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu
- Wanafunzi waliosajiliwa kwa mitihani ya ACCA
- Wanafunzi wa CIMA
Gharama
Wanafunzi waliosajiliwa kwa kufanya mitihani ya Bodi hawalipi gharama yoyote ya kutumia Maktaba.
Watumiaji wengine, wanafunzi toka vyuo vya Elimu ya juu, wanafunzi wa wanataaluma toka nje ya nchi hulipa Tsh. 3000/- kwa siku ndani ya muda wa kazi na hutozwa Tsh.2000/- zaidi baada ya muda wa kazi. Katika mihula mirefu ya masomo, maktaba iko wazi kwa umma wote mpaka saa nne usiku.
Sheria na Taratibu za Maktaba
Ili kutunza nidhamu, Maktaba ya NBAA imeweka taratibu na sheria mbalimbali ili watumiaji wa maktaba hiyo waweze kuzifuata. Taratibu na sheria hizi zina lengo la kuweka mazingira ya utulivu ya kujisomea kwa watumiaji wote.
Taratibu na sheria hizo ni kama zifuatazo:-
1. Kuzingatia ukimya ili kuruhusu wasomaji kuwa makini na kusoma. Hivyobasi kwakuweka hali hiyo ya ukimya, watumiaji wanatakiwa kuzima simu zao zisitoe mlipo na kuziweka katika hali ya ukimya (Silent mode) kwa muda wote wanaokuwepo eneo la Maktaba.
2. Watumiaji wa maktaba wanatakiwa wasirudishe vitabu kwenye makabati kwani kazi hii hufanywa na mfanyakazi wa Maktaba.
3. Kuvuta, kula na kunywa hakuruhusiwi ndani ya Maktaba.
4. Matumizi ya vyombo vyovyote vinavyotoa moto hayaruhusiwi.
5. Mikoba yenye ukubwa wa kuanzia 8”x5” hairuhusiwi.
6. Koti kubwa haziruhusiwi ndani ya maktaba.
7. Watumiaji wa maktaba wanatakiwa kuvaa kistaarabu kiasi cha kutosababisha chukizo au madhara kwa wengine. Kuvua shati, kuweka miguu juu ya samani na uvaaji wa viatu virefu hairuhusiwi.
8. Karatasi za kuandikia zinaruhusiwa, Jalada za vitabu na vitabu vingine haviruhusiwi ndani ya maktaba.
9. Msaidizi wa maktaba katika dawati la maelekezo/mapokezi, atasisitiza kukagua mikoba yote kabla ya kuondoka maktaba ili kuzuia utoaji wa vitabu usuoruhusiwa. Waazimaji wa itabu wanatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwenye hili.
10.Vyakula, vinywaji na matunda ya aina yoyote hairuhusiwi kwani inaweza kuvutia wadudu.
11.Wizi hauruhusiwi, mtu akikamatwa kwa kosa la wizi atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kutolewa taarifa polisi.
12.Kompyuta za maktaba zitumike kutafutia taarifa za masomo tu.
13.Watumiaji wa maktaba wanatakiwa wawe katika hali ambayo haizuii shughuli/utendaji kazi wa maktaba.
14.Watumiaji au waazimaji wa vitabu,watawajibika kwa uharibifu/upotevu wa kifaa chochote cha maktaba.
15.Watumiaji au waazimaji wa vitabu, watatakiwa kulipa thamani kamili ya kifaa kilichoharibika au kupotea. Ili kujua thamani ya kifaa kilichoharibika au kupotea, yafuatayo yatazingatiwa: -
1.Gharama ya sasa ya kifaa hicho
2.Faini ya dola za kimarekani 15.00
16.Watumiaji wa maktaba wanatakiwa kufuata sheria za maktaba. Maktaba ina haki ya kumsimamisha mtu yeyote asiyefuata sheria na wenye madeni kutumia maktaba.
Muda wa kufungua Maktaba
Siku | Muda wa kufungua |
Jumatatu mpaka Ijumaa | 3:00 asubuhi mpaka 10:00 jioni |
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu za Kitaifa | Maktaba hufungwa |
Wakati wa kipindi cha mitihani, Maktaba hufunguliwa kwa muda mrefu kama ifuatavyo: -
Siku | Muda wa kufungua |
Jumatatu mpaka Ijumaa | 3:00 asubuhi mpaka 2:00 usiku. |
Jumamosi | 3:00 asubuhi mpaka 10:00 jioni. |
Jumapili na Sikukuu za Kitaifa | Maktaba hufungwa |
Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia library@nbaa.go.tz au info@nbaa.go.tz