Taratibu za mtihani

Taratibu za Mitihani

Jinsi ya kuomba kujiunga na mitihani

Ingia kwenye mfumo wa usajili wa wanachama na wanafunzi (MEMS) ulio kwenye mtandao wa Bodi na fuata maelekezo

Maandalizi ya kujisomea

Bodi inasajili na kusimamia taasisi za kuendesha masomo ya mapitio kwa watahiniwa wanaojiandaa kwa mitihani ya Bodi . Taasisi hizi zinajulikana kuwa watoa mafunzo.

Watahiniwa wanatakiwa kuhudhuria masomo ya mapitio kwa watoa mafunzo waliosajiliwa ili wajiandae vya kutosha kwa mitihani ya bodi. Watahiniwa wanashauriwa kuhudhuria marejeo ya masomo kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kufanya mitihani ya bodi.

Barua ya udahili wa mitihani

Bodi inatoa barua ya udahili wa mitihani kwa watahiniwa wenye sifa za kufanya mitihani katika muhula husika kabla ya kuanza kwa mitihani. Kwa watahiniwa wanaoishi Dar es Salaam na Dodoma waende kuchukua barua zao za mtihani wenyewe katika ofisi za Bodi zilizopo katika mikoa/majiji hayo. Kwa watahiniwa waliochagua vituo vya mitihani nje ya Dar es salaam na Dodoma, barua zao za mitihani watatumiwa kwenye anuani zao za posta.

Uahirishwaji wa mitihani

katika kuahirisha mtihani mtahiniwa anatakiwa kufuata taratibu za uahirishwaji zilizoelekezwa.

Maombi ya kitambulisho

Mtahiniwa aliyepoteza au anataka kupata kitambulisho kipya baada ya cha zamani kuisha muda wake, anatakiwa kufanya yafuatayo:-

  • 1.Pakua na jaza fomu ya maombi ya kitambulisho.
  • 2.Lipia Tsh. 20,000/- kupitia kwenye mfumo wa malipo
  • 3.Wasilisha picha tatu za rangi zinazofanana
  • 4.Ambatisha risiti ya malipo pamoja na fomu ya ya maombi iliyojazwa kikamilifu
  • 5.Wasilisha fomu yako ya maombi Bodi wewe mwenyewe au kwa kutuma kupitia sanduku la barua.
  • 6.Kwa watahiniwa wanaoishi Dar es salaam na Dodoma watachukua vitambulisho vyao katika ofisi za NBAA wiki mbili kabla ya tarehe ya mtihani. Watahiniwa wengine wanatakiwa kuchukua vitambulisho vyao katika vituo vya mitihani siku moja kabla ya tarehe ya mtihani.

Kukata rufaa

Kwa mtahiniwa anayetaka kukata rufaa, aingie kwenye mfumo wa wanachama na wanafunzi (MEMS) unaopatikana katika tovuti ya Bodi na kufuata maelekezo