Majukumu ya kisheria

Kwa mamlaka ya sheria ya uanzishaji, [sheria ya wahasibu na wakaguzi (usajili) (sura ya 286 RE: 2002) kama ilivyoelezwa chini ya kifungu cha 4, Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA)

Ina mjukumu na mamlaka yafuatayo:

 • Kuendeleza na kutoa fursa na nyenzo za kuchunguza, kufundisha, uhasibu, ukaguzi na masomo shirikishi;
 • Kuendesha mitihani na kutoa diploma, vyeti na tuzo nyingine za Bodi katika uhasibu, ukaguzi na masomo shirikishi.
 • Kudhamini, kupanga na kutoa nyenzo kwa ajili ya mikutano semina na majadiliano, na ushauri kuhusu mambo yanayohusu uhasibu na masomo shirikishi
 • Kupanga kwa ajili ya uchapishaji na usambazaji wa jumla wa machapisho yaliyotokana na shughuli za bodi
 • Kueleza viwango na miongozo ya uhasibu au ukaguzi kadiri inavyofaa na kuhakikisha utimizwaji wa viwango na miongozo kwa masomo husika.
 • Kutunza rejesta ya wakaguzi, wahasibu, watunza vitabu na kampuni/mashirika yanayofanya kazi hizo.
 • Kufikiria na kuamua maombi ya usajili na kufanya usajili wa wakaguzi, wahasibu, watunza vitabu na kampuni/mashirika yanayofanya kazi hizo.
 • Kusimamia shughuli na mwenendo wa wakaguzi, wahasibu, watunza vitabu na kampuni/mashirika yanayofanya kazi hizo.
 • Kutathimini sifa za uhasibu wa nje kwa ajili ya kusamehewa sehemu ya mitihani ya Bodi.
 • Kutunga muundo wa uhasibu wa Taifa na mitaala ya mafunzo na kusimamia mitaala yote ya mafunzo ya uhasibu kwenye taasisi za mafunzo nchini kote inafuata muundo wa uhasibu wa Taifa
 • Kutathimini sifa za uhasibu wa taasisi za ndani kwa ajili ya kusamehewa sehemu ya mitihani ya Bodi
 • Kufanya majukumu mengine baada ya kushauriana na Waziri

Majukumu ya kisheria ya Bodi yaliyotajwa hapo juu yamefupishwa kama ifuatavyo:-

 • Usajili
 • Usimamizi
 • Uendelezaji taaluma ya uhasibu
 • Uwekaji Viwango
 • Kufanya majukumu mengine baada ya kushauriana na Waziri