Msamaha kwa Taasisi
Katika kuratibu na kusimamia mafunzo ya taaluma ya uhasibu nchini, Bodi inatambua na kukagua masomo yote ya uhasibu yanayotolewa na taasisi za mafunzo ya Uhasibu zinazotambuliwa nchini.
Kila taasisi inayotambuliwa kutoa masomo ya Uhasibu na ambayo inahitaji msamaha wa masomo inatakiwa kukidhi mahitaji ya msamaha, kujaza fomu na kuiwasilisha Bodi.
Msamaha utatolewa kwa masomo ya uhasibu baada ya Bodi kujiridhisha kuwa taasisi imetimiza masharti yaliyoelezwa kwenye Sera ya Msamaha inayotoa maelekezo katika kutimiza masharti ya msamaha yaliyowekwa na Bodi. Orodha ya Taasisi zinazotoa mafunzo ya Uhasibu na zilizopewa msamaha imeorodheshwa, bofya hapa.