Mapitio ya Ubora wa Ukaguzi

Bodi imejiandaa kutekeleza jitihada mbali mbali zitakazosaidia kufuatilia ubora wa kazi kwa wanachama wake.

Mojawapo ya jitihada hizo ni kuandaa mfumo wa mapitio ya ubora wa ukaguzi kwa wanachama wake wanaofanya kazi za ukaguzi. Mfumo huu umekusudiwa kutoa utaratibu wa kutathimini uwepo na ubora wa sera ya kudhibiti ubora na taratibu/kazi zinazofanywa na kampuni zilizosajiliwa.