Diploma ya IPSAS
Lengo la kazi
Kutoa uelewa wa kina wa matumizi kwa vitendo ya viwango vya kimataifa vya uhasibu wa sekta ya Umma
Makundi Lengwa
Diploma ya IPSAS humnufaisha mtu yeyote anayehitaji uelewa wa matumizi ya viwango vya kimataifa vya uhasibu wa sekta ya Umma ndani ya sekta ya umma.
Sifa za kuingilia
Wenye cheti cha Certified Public Accountant (CPA) au kinacholingana, AU wenye shahada ya juu katika uhasibu, Fedha, kodi na masomo yaliyochaguliwa.
Muda wa Kozi
Kozi ina awamu mbili za miezi sita, yaani Februari hadi Agosti na Septemba hadi Februari kila mwaka.
Saa za mafunzo
Masomo ya jioni yanaendeshwa mara tatu kwa wiki ( Jumatatu, Jumatano na Ijumaa) kwa muda wa saa mbili kwa siku kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 1:00 usiku.
Ada
Ada ya mafunzo TZS. 1,000,000
Ada ya usajili TZS. 20,000
Ada ya mitihani TZS 480,000
Jumla TZS 1,500,000
Mahali:
Dar es Salaam, NBAA – Mhasibu House
Dodoma
Arusha
Zanzibar
Tunzo
Bodi inatoa Diploma ya IPSAS kwawale wanaomaliza na kufaulu mtihani wa mwisho wa kila kozi.