Fellow Certified Public Accountant ( FCPA ) / FCPA-PP

Mtu atastahili kupandishwa hadhi ya usajili na kuwa "Fellow Accountant" iwapo ataIridhisha Bodi kuwa amekuwa "Associate Certificate Public Accountant" au "Associate Certified Public Accountant in Public Practice" mwenye uzoefu mzuri wa utendaji kazi wa miaka saba kabla ya maombi yake kama "Fellow Certified Public Accountant" au "Fellow Certified Public Accountant in Public Practice" na ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya taaluma wa Uhasibu ikiwemo:-

Kuwashauri angalau Wahasibu Wahitimu 20 katka kipindi cha miaka saba.

Utayarishaji na uwasilishaji wa angalau makala tano kuhusiana na taaluma ya uhasibu katika mkutano wa Utunzaji Hesabu au Ukaguzi

Kuchapisha angalau makala tatu kwenye Jarida la Uhasibu la NBAA

Hatimaye Mtu huyo anaweza kujaza fomu ya maombi na kuirudisha kwa ajili ya tathimini.