Utafiti
Utafiti ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Maarifa mapya na kazi za ubunifu hubadilisha ulimwengu, kujenga mustakabali na kuleta ukuaji endelevu wa Taifa. Kitengo cha utafiti cha NBAA, kina jukumu la kuratibu utafiti kwa lengo la kusimamia shughuli na mwenendo wa taaluma zaidi ya hayo, kushirikiana na wabia wengine kwenye maswala yanayohusu utafiti.
Vipaumbele vya utafiti
Vipaumbe vya utafiti vya NBAA vinaamuliwa na mahitaji ya mada mahususi, dhamira zinazoonekana na msaada kutoka kwa Idara husika na wadau wengine wanaofanyiwa utafiti. Hata hivyo kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuleta kipaumbele cha utafiti ambazo ni:
Maagizo ya Bodi ya Wakurugenzi
Masuala ya Uhasibu ya Taifa yenye maslahi kwa umma
Mpango wa kitengo cha Utafiti kwa mwaka
Utaratibu wa Utafiti
Kwa kawaida michakato au taratibu za utafiti wa sayansi za jamii ni zile zile, tofauti pekee iliyopo inayoweza kuonekana ni mbinu. Kwa mtazamo huu, michakato au taratibu za tafiti zetu zinazingatia yafuatayo: -
Ubainishaji wa tatizo la utafiti
Matayarisho ya mapendekezo ya utafiti yatakayojumuisha yafuatayo: -
Historia ya tatizo la utafiti
Malengo
Uhalali wa utafiti
Mbinu
Mpango kazi
Bajeti ya Utafiti
Ukusanyaji data
Uchanganuzi wa data
Utoaji taarifa
Upangaji Utafiti na mahitaji
Utafiti unafanywa kwa kuzingatia muundo unaoeleweka wa shabaha, majukumu na viashirio, Utaratibu wa karibu wa shughuli za utafiti utawezekana tu iwapo kuna mipango inayoeleweka. Kwa hiyo, upangaji utafiti na mahitaji ya NBAA, ni pamoja na .
Kuandaa nyaraka za utafiti , kwa mfano, Dodoso na fomu za kukusanyia data, tathimini na takwimu.
Kuhudhuria shughuli zote na mawasiliano kuhusu masuala ya utafiti na kudurusu ripoti za utafiti
Kutayarisha orodha hakiki ya masuala ya utafiti
Kutayarisha mpango kazi unaoonesha bajeti
Matayarisho ya mahitaji yote kwa ajili ya ziara za ugani yakiwemo mahojianao ya kwenye simu na kupeleka barua
Kupanga mahitaji yote kwa ajili ya kazi za utafiti.
Machapisho ya Utafiti
Kwa kuwa madhumuni ya utafiti ni kupata maarifa mapya, kuwasilisha matokeo kwa njia ya machapisho na uhuru wa kuchapisha, ni lazima vilindwe kwa nguvu zote. Matokeo ya utafiti uliofanywa na NBAA yanaweza kupatikana kupitia tovuti ya NBAA, majarida na magazeti ya wahasibu, Maktaba ya NBAA, na kwa njia nyingine yoyote itakayoonekana inafaa. (Bofya hapa).