Huduma za ushauri

Huduma mbalimbali za ushauri zinatolewa na NBAA kwa sekta ya Umma, sekta binafsi na kwa watu mmoja mmoja wanaohitaji ushauri maalumu kuhusu matumizi ya viwango, mzunguko wa fedha na usimamizi wa mali. Wateja wa ushauri wanalipa ada kulingana na huduma waliyopewa au kwa asilimia ya mali inayosimamiwa.

Sehemu hii inakusudia kutoa taarifa za kina kuhusu aina mbalimbali za huduma za ushauri, taratibu na utekelezaji wa shughuli za ushauri kwa wadau mbalimbali.

Baadhi ya huduma zinazotolewa ni pamoja na: -

Kutoa huduma za mafunzo ya ndani kuhusu uhasibu, ukaguzi na masomo shirikishi ya taaluma kwa mfano kuwezesha mafunzo kuhusu sheria mpya na viwango.

Matayarisho ya miongozo ya vitendea kazi kwa sekta ya umma na binafsi kwa mfano mwongozo wa uhasibu, mwongozo wa ununuzi na rejesta za kujikinga na hatari.

Kutayarisha sera mahususi za utendaji wa makampuni

Kutoa huduma za ushauri katika matumizi ya viwango mbalimbali vya uhasibu. Kwa mfano: IFRSs, IPSASs, ISA, na TFAS.

Msaada katika kutayarisha mpango wa Biashara

Huduma za Ofisi ya Ajira

Huduma hii ipo kwa ajili ya kuwasaidia wanachama kutafuta kazi katika sekta mbalimbali za uchumi.

Pia husaidia mashirika ya aina zote kuajiri wahasibu na wakaguzi wanaotambulika kisheria na kusaidia wanachama kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira na matatizo mengine katika ajira.

Ada za Ushauri

Wateja wa ushauri wanalipa ada; hata hivyo, hii inategemea na aina ya huduma inayotolewa. Kutoa fedha za kutosha kulingana na makadirio ya gharama halisi ni muhimu kwa matumizi yenye ufanisi ya huduma za ushauri. Makadirio makini ya gharama za ushauri ni sehemu muhimu ya kuangalia katika kupanga gharama mbalimbali za huduma za ushauri.

Vifuatavyo ni vibainishi muhimu vinavyojumuishwa kwenye kupanga ada za ushauri:

Kitita cha mkutano

Viandikia

Ada ya wataalamu na wafanyakazi saidizi

Gharama za usafiri

Mawasiliano

Muda wa ushauri (Idadi ya siku)

Ushindani wa Soko la Ushauri

Ushauri ni lazima uvutie gharama itakayokuwa inabadilishwa kila baada ya muda

Tathimini ya Utendajikazi wa huduma za ushauri

Huu ni upimaji wa jinsi kazi za ushauri zinavyofanywa katika huduma za ushauri kwa ujumla. Lengo ni kuboresha utendajikazi wa huduma za ushauri mara kwa mara. Baada ya kukamilika kwa kazi ya ushauri, mteja/wateja lazima wajaze fomu za uthamini kwa madhumuni ya tathimini ya utendajikazi.

Vifuatavyo ni vipengele muhimu vya kuzingatiwa katika mchakato wa tathimini ya utendajikazi wa huduma za ushauri:-

Ubora wa kazi ya ushauri

Uwezo wa kukamilisha kazi kwa muda unaotakiwa

Uzoefu maalumu na weledi wa kiufundi katika aina mahususi ya ushauri

Mbinu ya kazi ya ushauri

Utumiaji wa habibu za rejea

ZINGATIA: Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na Idara ya Ufundi na Ushauri