Tangazo la Mnada
Imewekwa: Jul 09, 2021
Wananchi wote wanatangaziwa kwamba, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) itauza kwa njia ya mnada wa hadhara gari moja chakavu aina ya Toyota Land Cruiser Station Wagon GX-STD katika Mkoa wa Dar es salaam. Mnada utafanyika Mhasibu House, Mtaa wa Bibi Titi Mohamed, Upanga – Dar Es Salaam 23/07/2021 kuanzia saa 4:00 asubuhi. (Pakua Tangazo)
Masharti ya Mnada:
- Gari itauzwa kama lilivyo na mahali lilipo
- Mnunuzi atatakiwa kulipa papo hapo amana (deposit) isiyopungua asilimia ishirini na tano (25%) ya thamani ya gari, na kukamilisha malipo yote katika muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya mnada. Mnunuzi akishindwa kutimiza malipo yote katika muda uliopangwa, atakosa haki zote za ununuzi wa gari hilo na amana (deposit) yake haitarudishwa.
- Mnunuzi atakayeshindwa kulipa amana (deposit) ya asilimia ishirini na tano (25%) papo hapo atachukuliwa kuwa na nia ovu ya kuharibu mnada hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yake kwa mujibu wa Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Mnunuzi atatakiwa kuondoa gari alilonunua katika muda wa siku saba (7) tangu kukamilisha malipo.
- Ruhusa ya kukagua gari itatolewa siku mbili kabla ya tarehe ya mnada
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU
4 BARABARA YA UKAGUZI, “AUDIT HOUSE”, GHOROFA YA NANE
S.L.P. 1271
41104 TAMBUKARELI
DODOMA, TANZANIA
SIMU.:+255 26 2160170 - 4
BARUA PEPE: info@nbaa.go.tz
TOVUTI:www.nbaa.go.tz