UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU TANZANIA (NBAA)
Imewekwa: Dec 21, 2024
Kufuatia uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Shayo Temu uliofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba(Mb.), kwa mamlaka aliyonayo chini ya Aya ya 1(2) ya Jedwali la tatu la Sheria ya Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Sura 286 amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi kama ifuatavyo;
1.CPA Leonard Mkude
2.CPA Salhina Mkumba
3.CPA Indiael Kaaya
4.CPA Mwamini Tuli
5.CPA Zainab Msimbe
ambao uteuzi wao ni wa kipindi cha miaka mitatu (03) kuanzia tarehe 27 Septernba, 2024 hadi tarehe 26 Septemba, 2027.
6.CPA Aisha Kapande
7.CPA Paul Bilabaye
8.CPA Issa Masoud
9.CPA Fredrick Msumali
10. CPA John Ndetico
ambao uteuzi wao ni wa kipindi cha pili cha miaka mitatu (03) kuanzia tarehe 9 Novemba, 2024 hadi tarehe 8 Novemba, 2027.
Imetolewa Na:
Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano,
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA).