Watoa Mafunzo

Bodi husajili na kusimamia taasis zinazoendesha masomo ya mapitio kwa wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yake. Taasis hizi hujulikana maarufu kama watoa mafunzo (Tuition Providers). Kwa wanafunzi ambao wanatamani kufanya mitihani ya Bodi, wanatakiwa kuhudhuria masomo haya kwa muda wa miezi sita kabla ya kufanya mitihani.

Wanafunzi wanaweza kufanya masomo haya ana kwa ana ama kwa muda wa ziada kutegemea na chaguo la mtu husika. wanafunzi wanashauriwa kuhudhuria masomo kwa watoa mafunzo ambao wamesajiliwa na kutambuliwa na Bodi.

Watoa mafunzo wanaopenda kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaojiandaa kwa mitihani ya Bodi, wanatakiwa kupitia Muongozo wa Usajili kwa Watoa Mafunzo (Tuition Providers Registration Guide) ambao hutoa maelekezo jinsi ya kujisajili kama kituo cha kufundishia. Baada ya kusoma muongozo huo, Taasis itajaza fomu ya usajili na kuiwasilisha Bodi kwa ajili ya kufanyiwa tathimini.

Bodi huwataka watoa mafunzo wote waliosajiliwa kuwasilisha fomu ya mrejesho (Annual Return Form) kwa kila mwaka kwa ajili ya ufuatiliaji na tathimini.

Iwapo unahitaji taarifa kamili ya kituo cha mafunzo tafadhali bofya hapa.


Wakati unapojiandaa kwa mitihani, kuna njia mbalimbali za kufanya mafunzo ya mapitio. Unaweza kufanya mafunzo yako kwa kujiandikisha kwenye vituo vya watoa mafunzo na kutumia nyenzo nyingi za mafunzo na mbinu zinazotolewa na watoa mafunzo hao/. Hii ni mojawapo ya njia bora zaidi za kufanya mafunzo wakati wa matayarisho ya mtihani . wengi wa watoa mafunzo wanatoa mafunzo ya ana kwa ana wakati taasisi chache nazo hutoa mafunzo kwa njia ya masafa.

Inapendekezwa kuwa unapotaka kufanya mafunzo yako kwa mtoa mafunzo, unaweza kuchagua taasisi moja inayotambulika na Bodi. Ni lazima uongeze mafunzo yako kwa kuwa na mpango wa kujisomea utakaofuata wakati wa matayarisho ya mtihani. Watoa mafunzo wanaotambuliwa wanafuatiliwa na Bodi kuhakikisha kuwa wametimiza viwango vinavyotakiwa kufanya shughuli hiyo. Angalau mara moja kwa mwaka kuna warsha inayofanyiwa na watoa huduma za mafunzo kwa lengo la kuimarisha utoaji mafunzo. Iwapo unahitaji taarifa kamili ya kituo cha mafunzo tafadhali bofya hapa.